Historia Ya Muda – Mashahidi Wa Yehova

Historia ya Muda

1879 Charles Taze Russell alianza kuchapa gazetti Zion’s Watch Tower na Herald of Christ’s Presence.

1881 Walianzisha Watchtower Tract Society.

1886 Russell alichapa kitabu chake Divine Plan of the Ages (Mpango wa Mungu Kwa Vizazi).

1914 Vita vya Mageddon haikutimia kama walivyotabiri.

1916 Charles Russell alifariki.

1917 J. F. Rutherford alichukua nafasi ya Russell.

1920 Watch Tower walidai watu mamillioni wanaoishi sasa hawatakufa! Tena walitabiri ufufuo wa ulimwengu huu katika mwaka wa 1925.

1925 Watu kama Ibrahimu, Isaka na Yakobu hawakufufuka kama walivyotabiri.

1930 Walijenga nyumba “Beth Sarim” kule San Diego, California U.S.A. kwa ajili ya manabii wa zamani wa Mungu. Walidai manabii wa zamani watafufuka na watahitaji sehemu ya kuishi.

1931 Walichagua jina “Mashahidi wa Yehova” kwa mara ya kwanza.

1942 Rutherford alikufa. N. H. Knorr alichukua nafasi yake.

1950 Walianza kuchapa tafsiri yao ya maandiko, New World Translation. Walimwita Yesu kuwa mungu kati ya miungu mingi. Tena waliongeza neno “Yehova” kwenye Agano Jipya.

1968 Kwenye Watch Tower waliandika kwamba inawezekana Yesu atarudi katika mwaka wa 1975.

1975 Yesu hakufika.


Historia Kwa Ufupi

 1. Charles Taze Russell (1854-1916) wa Marekani alianza kufundisha watu kwamba Yesu yu karibu kusimamisha ufalme wake. Katika mwaka 1872 bk. wafuasi wake waliunda chama cha ushirika.
 2. Kabla ya kuhubiri ya kuwa Yesu atarudi katika mwaka wa 1874 bk., Ndugu Russell alikuwa Msabato. Lakini alipinga mafundisho ya William Miller kuhusu Yesu atarudi lini, na alianza kufundisha mafundisho yake ya kuwa Yesu atarudi lini.
 3. Aliweka mkao mkuu Pittsburgh, Pennsylvania mwaka wa 1872, na alifanya yeye mwenyewe awe rahisi. Katika mwaka wa 1909 alihamisha mkao mkuu mpaka Brooklyn, New York.
 4. Lakini hawakuitwa Mashahidi wa Mungu mpaka mwaka 1931. Wanadai mashahidi walikuwepo duniani tangu siku za Habili na wanadondoa Isa. 43:10-12; Ebr. 11; na Yn. 18:37 kama ni uthibitisho wa imani yao.
 5. Charles Taze Russell aliandika vitabu sita vinaitwa, Studies In The Scriptures. Vitabu vile vilijenga msingi wa imani ya Mashahidi.
 6. Rusell alikufa mwaka wa 1916 na Joseph Rutherford alichaguliwa awe rais wao wa chama cha uchapaji kinachoitwa Watchtower Bible and Tract Society.
 7. Rutherford aliandika vitabu vingi vinavyoeleza imani yao. Na ndio yeye aliyeandika kwamba, “watu mamilioni wanaoishi sasa hawatakufa.” Alikuwa na mana kwamba Yesu atarudi karibuni. Walakini Rutherford mwenyewe alikufa mwaka 1942 na mpaka sasa Yesu hajarudi!
 8. Yeye alifundisha kwamba Yesu aliaanza kutawala mwaka 1914 na alitakasa hekalu la Mungu mwaka wa 1917. Na alitufundisha ya kuwa tutakuwa na vita kuu (Har-Magedoni) na ndipo Yesu atakuja kwa watu wake.
 9. Bada ya kifo cha Rutherford ndugu N. H. Knorr alichaguliwa awe rais, 1942.
 10. Katika mwaka wa 1950 waliandika tafsiri yao wenyewe ya Biblia inayoitwa “New World Translation”, wakasema ni tafsiri iliyo sahihi.
 11. Pia mwanzilishi wao (Russell) alikuwa MHUNI sana, sio kidogo lakini SANA! (Aliyeanzisha madhehebu ya Mashahidi na kuandika vitabu sita vinavyoitwa “Majifunzo Ndani ya Maandiko”.) Katika kitabu cha “Churches of Today” uk. 97, tunaambiwa yafuatayo: “Alipelekwa mahakamani na mkewe akishitakiwa kuwa ni mzinzi! Kortini, alikiri mwenyewe kwamba alikuwa na wapenzi wengi. Basi, serikali iliamua kuwa ni haki kwa mkewe apewe talaka na kumwacha. Tena, serikali ilimwamuru Russell ampe mkewe fidia. Russell alidai kuwa hana fedha. Lakini, serikali ilipeleleza mambo yake ikagundua kuwa alikuwa na fedha za Marekani $317,000 ambazo alikuwa amezificha kwa ujanja! Hivyo, alishitakiwa na serikali kuwa ni mwongo!”

Kwa hiyo mwanzilishi wa Mashahidi ni Mwasherati, Mwongo na Mwizi! Sasa leo watu wana mwaminije huyo mwongo?

 

 

 

 


‘KUAMINI’ MAANA YAKE NINI?

“Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu,hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe nauzima wa milele” Yohana 3:16. Mstari huu ni moja ya mistari inayopendwa katika Biblia, na bado ni moja ya mistari ya Biblia iliyokosewa kueleweka. Sintofahamu hiyo hutokana na watu kuchanganya maana ya “kuamini”. Wengine hufundisha kuwa neno “amini” hapa humaanisha tu kumtambua Yesu kama mwokozi, na kwamba endapo wakifanya hivyo wanakuwa kwenye hali ya kuokolewa.

Neno “amini” katika Yohana 3:16 hutokana na neno la Kiyunani pisteuo, linalomaanisha ushawishi, tumaini la furaha, muunganiko wa utiifu. Neno “amini” katika Agano Jipya mara nyingi hubeba dhana ya utii. Neno hili pekee yake halimaanishi “saini ya kifikra.”

Mtu anaweza kutazama mazingira ambayo waziwazi Yohana 3:16 huangukia na ataweza kuona ushahidi kwamba katika mstari huu Yesu alimaanisha mambo mengi zaidi ya saini ya kifikra.  Mazingira yenyewe ni Yohana 3:1-21. Na katika mistari hii twajifunza mambo matatu ambayo nataka kuyazingatia:

 1. Ili mtu awe ndani ya Yesu, ni lazima azaliwe mara ya pili, kuzaliwa kwa maji na kwa roho, Yohana 3:1-8.
 2. Katika Yohana 3:14 kuna nukuu ya Musa kumwinua nyoka jangwani. Hata kale, waliomtenda Mungu dhambi, hawakukaa tu nyumbani huku wakiamini kuwa yule nyoka wa shaba angewaokoa. Kimsingi walitakiwa kuinuka, kutembea kutoka hemani mwao, ambapo yawezekana ilikuwa ni umbali wa maili kadhaa (kumbuka kulikuwa na kambi ya watu wapatao milioni tatu) ili kufika mahali palipokuwa na yoka wa shaba ili kumtazama ili wawe hai, Hesabu 21:9. Ni wazi kwamba katika wokovu wao kulikuwa na zaidi ya saini ya kifikra

3) Yesu alidhihirisha kwamba endapo unataka kuijia nuru, kulikuwa na jambo ambalo mtu ulitakiwa kulifanya, “Bali yeye aitendaye kweli huja kwenye nuru,” Yohana 3:21.

Tuelewe kutokana na Neno la Mungu kuwa imani ya Kibiblia huhusisha imani inayompelekea mtu kutumaini na kutii. Kushindwa kutumaini na kumtii Yesu ni kushindwa dhahiri kumpokea kama Bwana na mwokozi. “Na kwanini mwaniita Bwana, Bwana, walakini hamyatendi nisemayo?” Luka 6:46


Yesu Ni Nani?

Kuna watu wengi wanafundisha mambo mengi kinyume na maandiko. Na kosa moja kubwa wako wanaofundisha mapotofu kuhusu Yesu; ni watu mbali mbali wanafundisha kwamba “Yesu ni muungu, lakini siyo Mwenyezi Mungu, ambaye ni Yehova,” (Let God Be True, uka. 33). Na wanadai Yesu ni “mtu aliyeumbwa,” ambaye “ni nafsi kuu ya pili juu ya ulimwengu,” (Make Sure of All Things, uka. 207).

Mafundisho haya kuhusu Yesu ni kinyume na Agano la Kale na Agano Jipya. Agano la Kale linafundisha kwamba Yesu atakuwa tofauti na atakuwa na sifa tofauti kuliko wote. Atakuwa Mungu.

Na kuna mistari mitatu kutoka Agano la Kale inaonyesha kuwa Yesu — Mesia — atakuja na atakuwa Mungu katika mwili.

Isaya 7:14 – “Tazama, bikira atachukua mimba, atazaa mtoto mwanaume, naye atamwita jina lake Imanueli.” “Imanueli” maana yake ni “Mungu pamoja nasi.”

Mathayo 1:21-23 – Inaweka wazi Yesu ni Imanueli aliyeongolea, na Yeye ni kwa kweli Mungu yuko pamoja nasi.

Isaya 9:6 – “Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanaume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani.”

Mstari huu unaweka wazi kwamba Mesia, Yesu atakuwa mtawala na siyo mtawala tu bali atakuwa “MUNGU MWENYE NGUVU.” Na katika Isaya 10:21, Isaya alitumia maneno yale yale kuongelea kuhusu Yehova, “Mungu aliye mwenye nguvu.” Kwa hiyo Isaya kupitia Roho Mtakatifu anaweka sawa kwamba Yesu na Yehova ni “Mungu mwenye nguvu.”

Mika 5:2 – “Bali wewe, Bethlehemu Efrata, uliye mdogo kuwa miongoni mwa elfu za Yuda; kutoka kwako wewe atanitokea mmoja atakayekuwa mtawala katika Israeli; ambaye matokeo yake yamekuwa tangu zamani za kale, tangu milele.”

Mika anasema yule atakayetokea ni “tangu zamani,” yaani “tangu milele.” Mungu tu ni wa milele, na kama yule atatokea ni wa milele basi ni lazima Yeye ni Mungu.

Tena Agano Jipya linatufundisha Yesu ni Mungu!

Yohana 1:1-4 – “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika. Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu.”

Hapa kuna mistari mingine kwenye Agano Jipya (Yn. 1:14; 1 Yn. 1:1 na Ufu. 19:13) jina “Neno” ni “Logos” katika Kiyunani, na katika kila sehemu “Logos” ni Yesu. Na tunaweza kujua Yohana katika Yoh. 1:1-4 anaongea kuhusu Yesus kwa sababu ya mstari wa Yoh. 1:14 aliposema, “Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu,” Yohana alisema, “Neno alikuwa Mungu,” (1:1).

Siyo Yohana tu alifundisha Yesu ni Mungu, hata Paulo anafundisha Yesu ni Mungu.

Warumi 9:5 – “Na katika hao alitoka Kristo kwa jinsi ya mwili. Ndiye aliye juu ya mambo yote, Mungu, mwenye kuhimidiwa milele.”

Wafilipi 2:5-6 – “Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu; ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho.”

1 Timotheo 3:16 – “Na bila shaka siri ya utauwa ni kuu. Mungu alidhihirishwa katika mwili, akajulikana kuwa na haki katika roho, akaonekana na malaika, akahubiriwa katika mataifa, akaaminiwa katika ulimwengu, akachukuliwa juu katika utukufu.”

Tito 2:13 – “Tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu Mungu mkuu na Mwokozi wetu.”

Hata Yesu mwenyewe alisema Yeye ni Mungu.

Yohana 10:25-30 – “Yesu akawajibu, Naliwaambia, lakini ninyi hamsadiki. Kazi hizi ninazozifanya kwa jina la Baba yangu ndizo zinazonishuhudia. Lakini ninyi hamsadiki, kwa sababu hammo miongoni mwa kondoo wa mtu. Kondoo wangu waisikia sauti yangu; nami nawajua, nao wanifuata. Nami nawapa uzima wa milele; wala hawatapotea kamwe; wala hakuna mtu awezaye kuwapokonya katika mkono wa Baba yangu. Mimi na Baba tu umoja!”

Wayahudi walielewa maana ya Yesu alipomwita Mungu, “Baba yangu,” (mst. 25), alisema anauwezo wa kugawa uzima wa milele (mst. 28) na aliposema, “Mimi na Baba tu umoja!” (mst. 30). Tunajua Wayahudi walielewa Yesu alikuwa ana eleza Yeye ni Mungu, kwa sababu wakakusanya mawe ili wamuue, kwa sababu “Wewe uliye mwanadamu wajifanya mwenyewe u Mungu,” (Mst. 33).

Yohana 8:58 – “Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Yeye Ibrahimu asijakuwako, mimi niko.” Hapa tunaona Yesu anatumia maneno yale yale kuhusu mwenyewe, Yehova alitumia katika Kutoka 3:14. Na kwa sababu ya maneno haya Wayahudi walitaka kumpiga na mawe.

Yohana 14:8 – “Filipo akamwambia, Bwana, utonyeshe Baba, yatutosha.” Hapa tunaona Filipo aliomba Yesu amwonyeshe Baba, lakini angalia Yesu alijibu nini? Mstari 9, “Aliyeniona mimi amemwona Baba.” Mstari 10, “Husadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba na Baba yu ndani yangu?” Kwa hiyo Yesu aliweka wazi aliyeona Yeye ameshaonana na Baba.

Pia, tunajua Yesu ni Mungu kupitia uwezo wake

1. Tunaona katika Mathayo 14:33 watu walimwabudu Yesu na Yesu alipokea ibada yao. Tunajua tunatakiwa kuabudu Mungu tu (Yn. 4:24). Katika Ufunuo 22:8-9, malaika alikataa kuabudiwa, Mdo. 10:25-26, wanadamu walikataakuabudiwa. Lakini Yesu alipokea ibada yao, inathibitisha Yeye ni Mungu.

2. Katika Marko 2:5-11, Yesu alisame dhambi. Ni Mungu tu anauwezo wa kusamehe dhambi. Kwa kuwa Yesu anasamehe dhambi maana yake Yeye ni Mungu.

3. Katika Mathayo 28:18, Yesu alifundisha amepewa mamlaka yote! Mungu tu anayomamlaka yote kwa hiyo Yesu ni Mungu.

Tena, Hapa Baba (Yehova) Anafundisha Yesu ni Mungu! 

Waebrania 1:8 – “Lakini kwa habari za Mwana asema, Kiti chako cha enzi, Mungu, ni cha milele; na fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya adili.” Hapa kwa urahisi tunaona Baba (Yehova) anamwita Mwana, MUNGU!

Hitimisho

Kama utatambua Yesu ni Mungu na kufuata maagizo yake utaweza kupokea uzima wa milele. Kwa hiyo naomba kuwa wote wanaosoma watambue Yesu kama mtume Tomaso katika Yohana 20:28,

“Tomosa akajibu, akamwambia, Bwana wangu na Mungu wangu!”

Kwa msaada zaidi tunakukaribisha utuandikie:

kanisalakristo@yahoo.com

http://www.kanisalakristo.com