- Charles Taze Russell (1854-1916) wa Marekani alianza kufundisha watu kwamba Yesu yu karibu kusimamisha ufalme wake. Katika mwaka 1872 bk. wafuasi wake waliunda chama cha ushirika.
- Kabla ya kuhubiri ya kuwa Yesu atarudi katika mwaka wa 1874 bk., Ndugu Russell alikuwa Msabato. Lakini alipinga mafundisho ya William Miller kuhusu Yesu atarudi lini, na alianza kufundisha mafundisho yake ya kuwa Yesu atarudi lini.
- Aliweka mkao mkuu Pittsburgh, Pennsylvania mwaka wa 1872, na alifanya yeye mwenyewe awe rahisi. Katika mwaka wa 1909 alihamisha mkao mkuu mpaka Brooklyn, New York.
- Lakini hawakuitwa Mashahidi wa Mungu mpaka mwaka 1931. Wanadai mashahidi walikuwepo duniani tangu siku za Habili na wanadondoa Isa. 43:10-12; Ebr. 11; na Yn. 18:37 kama ni uthibitisho wa imani yao.
- Charles Taze Russell aliandika vitabu sita vinaitwa, Studies In The Scriptures. Vitabu vile vilijenga msingi wa imani ya Mashahidi.
- Rusell alikufa mwaka wa 1916 na Joseph Rutherford alichaguliwa awe rais wao wa chama cha uchapaji kinachoitwa Watchtower Bible and Tract Society.
- Rutherford aliandika vitabu vingi vinavyoeleza imani yao. Na ndio yeye aliyeandika kwamba, “watu mamilioni wanaoishi sasa hawatakufa.” Alikuwa na mana kwamba Yesu atarudi karibuni. Walakini Rutherford mwenyewe alikufa mwaka 1942 na mpaka sasa Yesu hajarudi!
- Yeye alifundisha kwamba Yesu aliaanza kutawala mwaka 1914 na alitakasa hekalu la Mungu mwaka wa 1917. Na alitufundisha ya kuwa tutakuwa na vita kuu (Har-Magedoni) na ndipo Yesu atakuja kwa watu wake.
- Bada ya kifo cha Rutherford ndugu N. H. Knorr alichaguliwa awe rais, 1942.
- Katika mwaka wa 1950 waliandika tafsiri yao wenyewe ya Biblia inayoitwa “New World Translation”, wakasema ni tafsiri iliyo sahihi.
- Pia mwanzilishi wao (Russell) alikuwa MHUNI sana, sio kidogo lakini SANA! (Aliyeanzisha madhehebu ya Mashahidi na kuandika vitabu sita vinavyoitwa “Majifunzo Ndani ya Maandiko”.) Katika kitabu cha “Churches of Today” uk. 97, tunaambiwa yafuatayo: “Alipelekwa mahakamani na mkewe akishitakiwa kuwa ni mzinzi! Kortini, alikiri mwenyewe kwamba alikuwa na wapenzi wengi. Basi, serikali iliamua kuwa ni haki kwa mkewe apewe talaka na kumwacha. Tena, serikali ilimwamuru Russell ampe mkewe fidia. Russell alidai kuwa hana fedha. Lakini, serikali ilipeleleza mambo yake ikagundua kuwa alikuwa na fedha za Marekani $317,000 ambazo alikuwa amezificha kwa ujanja! Hivyo, alishitakiwa na serikali kuwa ni mwongo!”
Kwa hiyo mwanzilishi wa Mashahidi ni Mwasherati, Mwongo na Mwizi! Sasa leo watu wana mwaminije huyo mwongo?
Leave a Reply