Kuna watu wengi wanafundisha mambo mengi kinyume na maandiko. Na kosa moja kubwa wako wanaofundisha mapotofu kuhusu Yesu; ni watu mbali mbali wanafundisha kwamba “Yesu ni muungu, lakini siyo Mwenyezi Mungu, ambaye ni Yehova,” (Let God Be True, uka. 33). Na wanadai Yesu ni “mtu aliyeumbwa,” ambaye “ni nafsi kuu ya pili juu ya ulimwengu,” (Make Sure of All Things, uka. 207).
Mafundisho haya kuhusu Yesu ni kinyume na Agano la Kale na Agano Jipya. Agano la Kale linafundisha kwamba Yesu atakuwa tofauti na atakuwa na sifa tofauti kuliko wote. Atakuwa Mungu.
Na kuna mistari mitatu kutoka Agano la Kale inaonyesha kuwa Yesu — Mesia — atakuja na atakuwa Mungu katika mwili.
Isaya 7:14 – “Tazama, bikira atachukua mimba, atazaa mtoto mwanaume, naye atamwita jina lake Imanueli.” “Imanueli” maana yake ni “Mungu pamoja nasi.”
Mathayo 1:21-23 – Inaweka wazi Yesu ni Imanueli aliyeongolea, na Yeye ni kwa kweli Mungu yuko pamoja nasi.
Isaya 9:6 – “Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanaume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani.”
Mstari huu unaweka wazi kwamba Mesia, Yesu atakuwa mtawala na siyo mtawala tu bali atakuwa “MUNGU MWENYE NGUVU.” Na katika Isaya 10:21, Isaya alitumia maneno yale yale kuongelea kuhusu Yehova, “Mungu aliye mwenye nguvu.” Kwa hiyo Isaya kupitia Roho Mtakatifu anaweka sawa kwamba Yesu na Yehova ni “Mungu mwenye nguvu.”
Mika 5:2 – “Bali wewe, Bethlehemu Efrata, uliye mdogo kuwa miongoni mwa elfu za Yuda; kutoka kwako wewe atanitokea mmoja atakayekuwa mtawala katika Israeli; ambaye matokeo yake yamekuwa tangu zamani za kale, tangu milele.”
Mika anasema yule atakayetokea ni “tangu zamani,” yaani “tangu milele.” Mungu tu ni wa milele, na kama yule atatokea ni wa milele basi ni lazima Yeye ni Mungu.
Tena Agano Jipya linatufundisha Yesu ni Mungu!
Yohana 1:1-4 – “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika. Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu.”
Hapa kuna mistari mingine kwenye Agano Jipya (Yn. 1:14; 1 Yn. 1:1 na Ufu. 19:13) jina “Neno” ni “Logos” katika Kiyunani, na katika kila sehemu “Logos” ni Yesu. Na tunaweza kujua Yohana katika Yoh. 1:1-4 anaongea kuhusu Yesus kwa sababu ya mstari wa Yoh. 1:14 aliposema, “Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu,” Yohana alisema, “Neno alikuwa Mungu,” (1:1).
Siyo Yohana tu alifundisha Yesu ni Mungu, hata Paulo anafundisha Yesu ni Mungu.
Warumi 9:5 – “Na katika hao alitoka Kristo kwa jinsi ya mwili. Ndiye aliye juu ya mambo yote, Mungu, mwenye kuhimidiwa milele.”
Wafilipi 2:5-6 – “Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu; ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho.”
1 Timotheo 3:16 – “Na bila shaka siri ya utauwa ni kuu. Mungu alidhihirishwa katika mwili, akajulikana kuwa na haki katika roho, akaonekana na malaika, akahubiriwa katika mataifa, akaaminiwa katika ulimwengu, akachukuliwa juu katika utukufu.”
Tito 2:13 – “Tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu Mungu mkuu na Mwokozi wetu.”
Hata Yesu mwenyewe alisema Yeye ni Mungu.
Yohana 10:25-30 – “Yesu akawajibu, Naliwaambia, lakini ninyi hamsadiki. Kazi hizi ninazozifanya kwa jina la Baba yangu ndizo zinazonishuhudia. Lakini ninyi hamsadiki, kwa sababu hammo miongoni mwa kondoo wa mtu. Kondoo wangu waisikia sauti yangu; nami nawajua, nao wanifuata. Nami nawapa uzima wa milele; wala hawatapotea kamwe; wala hakuna mtu awezaye kuwapokonya katika mkono wa Baba yangu. Mimi na Baba tu umoja!”
Wayahudi walielewa maana ya Yesu alipomwita Mungu, “Baba yangu,” (mst. 25), alisema anauwezo wa kugawa uzima wa milele (mst. 28) na aliposema, “Mimi na Baba tu umoja!” (mst. 30). Tunajua Wayahudi walielewa Yesu alikuwa ana eleza Yeye ni Mungu, kwa sababu wakakusanya mawe ili wamuue, kwa sababu “Wewe uliye mwanadamu wajifanya mwenyewe u Mungu,” (Mst. 33).
Yohana 8:58 – “Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Yeye Ibrahimu asijakuwako, mimi niko.” Hapa tunaona Yesu anatumia maneno yale yale kuhusu mwenyewe, Yehova alitumia katika Kutoka 3:14. Na kwa sababu ya maneno haya Wayahudi walitaka kumpiga na mawe.
Yohana 14:8 – “Filipo akamwambia, Bwana, utonyeshe Baba, yatutosha.” Hapa tunaona Filipo aliomba Yesu amwonyeshe Baba, lakini angalia Yesu alijibu nini? Mstari 9, “Aliyeniona mimi amemwona Baba.” Mstari 10, “Husadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba na Baba yu ndani yangu?” Kwa hiyo Yesu aliweka wazi aliyeona Yeye ameshaonana na Baba.
Pia, tunajua Yesu ni Mungu kupitia uwezo wake
1. Tunaona katika Mathayo 14:33 watu walimwabudu Yesu na Yesu alipokea ibada yao. Tunajua tunatakiwa kuabudu Mungu tu (Yn. 4:24). Katika Ufunuo 22:8-9, malaika alikataa kuabudiwa, Mdo. 10:25-26, wanadamu walikataakuabudiwa. Lakini Yesu alipokea ibada yao, inathibitisha Yeye ni Mungu.
2. Katika Marko 2:5-11, Yesu alisame dhambi. Ni Mungu tu anauwezo wa kusamehe dhambi. Kwa kuwa Yesu anasamehe dhambi maana yake Yeye ni Mungu.
3. Katika Mathayo 28:18, Yesu alifundisha amepewa mamlaka yote! Mungu tu anayomamlaka yote kwa hiyo Yesu ni Mungu.
Tena, Hapa Baba (Yehova) Anafundisha Yesu ni Mungu!
Waebrania 1:8 – “Lakini kwa habari za Mwana asema, Kiti chako cha enzi, Mungu, ni cha milele; na fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya adili.” Hapa kwa urahisi tunaona Baba (Yehova) anamwita Mwana, MUNGU!
Hitimisho
Kama utatambua Yesu ni Mungu na kufuata maagizo yake utaweza kupokea uzima wa milele. Kwa hiyo naomba kuwa wote wanaosoma watambue Yesu kama mtume Tomaso katika Yohana 20:28,
“Tomosa akajibu, akamwambia, Bwana wangu na Mungu wangu!”
Kwa msaada zaidi tunakukaribisha utuandikie:
kanisalakristo@yahoo.com
http://www.kanisalakristo.com